Ockoba 29, 2020
Ndugu Familia,
Nina matumaini barua hii inawakuta mkiwa salama. Kama mjuavyo, tunafikia mwisho wa robo tatu ya kwanza ya mwaka wa masomo ifikapo Novemba 2. Wiki moja baadaye siku ya Novemba 9. Kadi za ripoti zitatumwa nyumbani. Kila kadi ya ripoti itatoa maelezo ni jinsi gani mwanafunzi amefanya katika kazi za masomo na pia taarifa juu ya mahudhulio. Ripoti pia itakuwa ni kichocheo cha mazungumzo, na tunakualika wewe kuwasiliana na walimu na watumishi kwa taarifa zaidi na maelekezo ukiwa unatafuta njia za kusaidia masomo na kufanya vizuri kweenye masomo.
Kazi za ripoti kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa robo tatu ya kwanza itajumuisha taarifa za matokeo kwa mfumo wa maelezo na haitakuwa na maksi kama ilivyo kawaida. Maoni haya kwa maelezo yatatoa taarifa maalumu kuhusu taaluma na tabia na kujuisha maelezo ya maeneo anayofanya vizuri na maeneo ambayo yanampa changamoto.
Kadi kwa wanafunzi wa Sekondari itakuwa na maksi pamoja na baadhi ya maelezo. Maksi zinalenga kwa ujumla ni jinsi gani mwanafunzi wako alielewa masomo aliyo fundishwa. Kumbuka kwamba, katika baadhi ya hali, maksi kwa robo tatu hii inaegemea na taarifa chache. Lakini, katika hali yote, kufanya vizuri kunaweza kuboreshwa na kuwa imara.
Kama unahitaji msaada wa kutafsiriwa kadi ya ripoti, tafadhali wasiliana na mratibu wa mahusiano ya familia na shule anayeongea kiswahihi ama piga simu kwenye ofisi ya Mahusiano ya Jamii na Familia kwenda (540) 437-5017.
Tunatambua kuwa ujifunzaji wa mbali ni changamoto kwa karibia wanafunzi wote. Kadiri wakati unavyozidi kwenda, wanafunzi na waalimu wamezoea mazoea mapya, matarajio wazi, na kusuluhisha shida na zana za teknolojia. Tunaendelea kufanya juhudi kubwa kusaidia mahitaji ya kijamii na kihemko ya wanafunzi na kujibu mahitaji ya familia kwa msaada wa kiteknolojia na ujifunzaji. Tafadhali jua kwamba tunathamini maoni unayotoa. Tafadhali endelea kuungana nasi. Pamoja, tunaweza kutoa njia ya mafanikio.
Nawatakia Mema,
J. Patrick Lintner
Afisa Mkuu wa Taaluma